Skip to main content

MASOMO YA MISA JUMAPILI, AGOSTI 28, 2022. DOMINIKA YA 22 YA MWAKA ( Sunday Mass Readings)

MASOMO YA MISA 
JUMAPILI, AGOSTI 28, 2022
DOMINIKA YA 22 YA MWAKA

SOMO 1
YbS 3:17 – 20, 28 -29

Mwanangu, wakati wa kufanikiwa uendelee katika unyenyekevu; hivyo utapendwa kuliko mwenye ukarimu. Kadiri ulivyo mkuu uzidi kujinyenyekesha, nawe utapata kibali machoni pa Bwana; kwa maana rehema zake Bwana zi kuu, na siri yake ni kwa wanyenyekevu.

Msiba wa mwenye kiburi hauleti kupona, Mche wa uovu umepandika ndani yake. Moyo wa busara utatambua mithali, Na sikio sikivu ni tamaa ya mtaalamu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 68:3 – 6, 9 – 10 (K) 10

(K) Ee Mungu, Kwa wema wako uliwahifadhi walioonewa.

Wenye haki watafurahi,
Na kushangilia uso wa Mungu;
Naam, watapiga kelele kwa furaha.
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake.
Furahini katika Bwana, shangilieni mbele zake. (K)

Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,
Mungu katika kao lake takatifu.
Mungu huwakalisha wapweke nyumbani,
Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa. (K)

Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema,
Urithi, urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.
Kabila lako lilifanya kao lake huko,
Ee Mungu,
Kwa wema wako uliwahifadhi walioonewa. (K)

SOMO 2
Ebr. 12:18 – 19, 22 – 24

Hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliwaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani, na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lolote linguine. Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Mt. 11:25

Aleluya, aleluya,
Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, 
kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, Ukawafunuliwa watoto wachanga.
Aleluya.

INJILI
Lk. 14:1, 7 – 14

Yesu alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema, Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe, akaja yule aliyewaalika wewe nay eye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma. Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele Zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

Comments

Popular posts from this blog

Cancel Culture: Modern Justice or Online Bullying?

  In today’s digital age, cancel culture seems to stir up more heated debate than most. Some hail it as a way for society to hold public figures and institutions accountable while others see it as a dangerous form of online bullying; an unforgiving, mob-driven take-down with real-life consequences. But what exactly is cancel culture, and is it helping or hurting our world? Let’s explore both sides of the coin. Cancel Culture as Modern Justice One of the strongest arguments for cancel culture is that it gives power to the powerless. For generations, marginalised voices were silenced by systems that protected the rich, the famous, and the powerful. Today, social media has changed that. When someone speaks out about racism, sexism, abuse, or corruption, their voice can echo around the globe within hours. The public can demand change and more importantly, demand accountability. Consider cases where traditional institutions failed to act until social pressure forced them to. In these mo...

Men vs. Women: Do We Really Listen Differently?

Have you ever told a story to a guy, expecting an emotional reaction, only to get a “Hmm… that’s rough” in response? Or maybe you’ve shared something with a woman, and she immediately started asking ten follow-up questions about how you felt? If so, congratulations—you’ve witnessed firsthand how men and women often listen in very different ways. But why does this happen? Is it just personality differences, or is there something deeper at play? Let’s dive into the fascinating world of how men and women listen. Men: The Fixers For many men, listening is a mission. The goal? Find the problem and solve it. When a guy hears someone venting about a tough day, his brain starts scanning for solutions: ✅ “Did you try talking to your boss?” ✅ “Maybe you should switch gyms.” ✅ “Here’s what I would do…” This isn’t because men don’t care—it’s actually the opposite. They think the best way to help is to fix whatever’s wrong. The issue? Sometimes, the person talking doesn’t want a solution; ...

Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu Lyrics

By G.A Chavalla,  St. Maurus Kurasini. Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu, (nani angesimama)*3 mbele yako. 1. Lakini kwako kuna msamaha, ili wewe uogopwe, nimemngoja Bwana, roho yangu, na neno lake nimelitumaini. 2. Nafsi yangu inamngoja Bwana, kuliko walinzi, walinzi waingojavyo asubuhi Naam walinzi waingojavyo asubuhi. 3. Ee Bwana toka vilindini, nimekulilia. Bwana sauti yangu usikie, masikio yako yasikie Dua zangu.