By G.A Chavalla, St. Maurus Kurasini.
Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu, (nani angesimama)*3 mbele yako.
1. Lakini kwako kuna msamaha, ili wewe uogopwe, nimemngoja Bwana, roho yangu, na neno lake nimelitumaini.
2. Nafsi yangu inamngoja Bwana, kuliko walinzi, walinzi waingojavyo asubuhi Naam walinzi waingojavyo asubuhi.
3. Ee Bwana toka vilindini, nimekulilia. Bwana sauti yangu usikie, masikio yako yasikie Dua zangu.
Comments
Post a Comment